Luke 23:44-49

Kifo Cha Yesu

(Mathayo 27:45-56; Marko 15:33-41; Yohana 19:28-30)

44 aIlikuwa kama saa sita mchana, nalo giza likafunika nchi yote hadi saa tisa, 45 bkwa sababu jua liliacha kutoa nuru. Pazia la Hekalu likachanika vipande viwili. 46 cYesu akapaza sauti yake akasema, “Baba, mikononi mwako naikabidhi roho yangu.” Baada ya kusema haya, akakata roho.

47 dYule jemadari alipoona yaliyotukia, akamsifu Mungu, akasema, “Hakika, mtu huyu alikuwa mwenye haki.” 48 eWatu wote waliokuwa wamekusanyika hapo kushuhudia tukio hili walipoyaona hayo, wakapigapiga vifua vyao kwa huzuni na kwenda zao. 49 fLakini wale wote waliomfahamu, pamoja na wale wanawake waliokuwa wamemfuata kutoka Galilaya, walisimama kwa mbali wakiyatazama mambo haya.

Copyright information for SwhNEN